Maria Immakulata, Mama wa Kanisa,

Sisi tuliokusanyika hapa kwa shukrani tunakumbuka mchango wako kwa kazi ya Oasis ya Kanisa Hai.

Kwa shukrani tunakiri kwamba ni kwa upendo wako, Mafungo (Oasis) ya kwanza ya Maria Immakulata, ambayo yalikabidhiwa usimamizi wako maalum baada ya kubuniwa kwa namna ya ajabu ndani ya kikundi cha Oasis kisha kwenye kikundi cha Mwanga-Maisha.

Tunakiri kwamba mtazamo wako usio na kiasi, kujitolea kwako kuwa mwenzi wa Kristu kwa njia ya upendo ndiyo chanzo cha uzazi wako kati ya watu wa Mungu. Kwa kuwa ndiwe Immakulata Bi-arusi wa neno, hasa kwa ushirika naye Kristu katika saa ya upendo mkuu Msalabani, ndiwe Mama wa wote walio hai na Mama wa Kanisa

Pia tunakiri kwamba tukiwa kwenye ushirika nawe katika mtazamo wa ibada ya mwenzi wa Kristu ndiyo na itabaki daima kuwa kanuni pekee ya kweli na ya ndani kabisa ya uhai na uzazi ya Mama Mtakatifu wa Kanisa. Kanisa litakuwa Mama Kanisa pamoja nawe iwapo tu katika washiriki wake fulani, atakuwa pamoja nawe Bibi-arusi aliyejitoa kwa Bwana kwa imani na upendo.

Tunaamini kwamba kazi nzima ya Oasis inaendana na uelewa wa fumbo hili na haina lengo lingine zaidi ya kuwainua washiriki wake kwa uelewa wa kina kila wakati na utekelezaji wa mtazamo wa kujimiliki wenyewe katika kujitoa zawadi ya kweli kwa Kristo na kwa ndugu zao.

Tunaamini kwamba mtazamo huo ndio chanzo cha maisha mapya; hii ndiyo sababu tunakukabidhi kazi hii, kwa undani na uangalifu zaidi, tunakusihi kwa unyenyekevu kukubali na kuifanya kazi hii kuwa yako mwenyewe.

Tunaamini kwamba tutakuwa “Oasis ya Kanisa Hai” ikiwa tu tutaungana nawe katika kutekeleza mtazamo wa huduma na wakfu kwa Kristo katika Kanisa lake.

Hivyo basi, tunaomba uwapokee kama mali yako, wale wote ambao wametoa maisha yao na nguvu zao zote kwa Diakonia ya Kikundi cha Mwanga-Maisha.

Wapokee wote, hasa wasimamizi na wahuishaji ambao, ndani ya kikundi hiki, wamependezwa kuitumikia kazi kuu ya kujenga jumuiya zinazofanya kazi ya Kanisa.

Wapokee kama mali yako pia wale wote ambao mwisho wa mafungo yao ya Oasis wamekabidhi maazimio yao mikononi mwako na uwape neema ya kustahimili.

[Pokea pia mahali hapa kama mali yako mwenyewe, ambamo kila kitu ni cha kuitumikia kazi ya Oasis ya Kanisa Hai, pafanye paitumikie sababu hii bila vizuizi vyovyote.]

Maria Immakulata, Mama wa Kanisa, ukawe pia Mama wa kazi ya Oasis na Kikundi cha Mwanga-Maisha.

Amina.